Thursday, 26 March 2009

No waterzzzzzzzzzzz




Hapa ndiyo tuone usawa unavyokosekana, ndiyo maana wananchi tunashindwa kuvumilia kutokana na shida hizi. Picha hii inaonesha bomba la maji maeneo ya manzese likiwa limefungwa kutokana na sababu kuwa maji hakuna. je pesa zote hizi ambazo kuna baadhi ya vigogo wanazichezea kwa kulewa na kujenga majumba ya kifahari kwanini zisitumike katika kuendesha huduma kama hizi. Maji yamekuwa shida sana, lakini bado tunayahitaji.

YAANI KWA UPANDE WANGU SIELEWI KABISA. ILA SISI WATANZANIA NI WAOGA SANA KATIKA SUALA LA KUHOJI ILI TUJUE HAKI ZETU.

5 comments:

  1. Ona kwanza Ngurdoto Mountain Lodge, Arusha-Tanzania iliyowekwa kwenye blog kwanza. Sasa rudi haoa kwenye picha ya Manzese, kama moyo au roho yako haiguswi basi jua una matatizo mengi au Mungu alimweka mbali na wewe muda mrefu.

    Angalieni mfano wa india, gap between the rich and the poor astronomical, angalia China kila mtu ana kazi, masikini/tajiri wengi wanakazi kazi fulani,linganisha vurugu katika hizo nchi, china inajua jinsi ya kutuliza vurugu kabla hata hazijawa kubwa, jeshi lao ni imara mno. huko India hata mapolisi wanaungana na wanaofanya vurugu.

    Masikini mpe kazi basi kuondoa mawazo yake, awe busy na shughuli, maendeleo hayaji hivi hivi lazima mtu usote,(zaidi kama wewe ni masikini) ukisha kubali huo ukweli ndio utaishi kwa amani, hata kama wewe hautafanikiwa basi hakikisha watoto wanasoma,wanafanya vizuri maishani, kila kitu kina mwanzo, kwa nini wewe usiwe mwanzo wa kuikomboa familia yako, achana na anasa, ulevi, ..... Angalia maisha yako kwanza, acha ndoto utaishia kuiba ukidhani ndio utajijenga (siku za mwinzi ni...) Hakuna mtu atayemshikia mtu fimbo kumwambia ajiendeleze, tena kwa taarifa yako matajari na wajanja wengi wanategemea watu kuendelea kuwa masikini na wajinga ili wao wanufaidike.

    Huku manzese ni kwa walala hoi, (samahani kama unaishi huko) lakini haki yao wapewe, kufungiwa maji ni kuipa mzigo serikali ambayo iko busy na mambo mengine ya kimaendeleo, siku watu wataamua potelea pote na amani ndio itavurugika hapo, kibali cha kukata maji wamekitoa wapi? Nani alidhiinisha upande wa wadaiwa? Serikali ilikuwa inajua kuhusu hatua za kukata maji? Mambo nchini yanafanyika bila kuzingatia utaratibu, kona nyingi kwa wanaozijulia. Urasimu unafaa katika mazingira kama haya ya watu kukosa maji.Asubuhi njema.

    ReplyDelete
  2. hali ikiendelea hivi, mwakani CCM hawapati kitu kwenye kura. MTU MWENYE AKILI AWEZI KUWAPIGIA KURA CCM. cheki hali ya maisha ilivyokuwa ngumu. wakati wananchi tunateseka, viongozi wanazidi tu kushindana kununua magari na majumba ya kifahari. je tutafika?

    ReplyDelete
  3. HIVI NI VITUKO USAHILINI, AH! USWAHILINI KUNA VITUKO, MMMHH
    MI SIWEZI KUISHI HUKU.

    ReplyDelete
  4. MIMI PIA SIWEZI KUISHI UKU.UCHUNGU MTUPU

    ReplyDelete
  5. HUKU WANAOISHI NI MBWA KOKOZZ MIMI SIWEZI KUKAA HUKU HATA IWEJE. DUUU KWELI NI VITUKO USWAHILINI.

    ReplyDelete

SEMA USIOGOPE, JAMII INAKULINDA.