NOOMBA NIANZISHE MJADARA HUU AMBAO LABDA UTASAIDIA NCHI YETU. JAMAMI WATANZANIA WENZANGU, NAOMBA MKUBALIANE NA MIMI YA KUWA SISI NI WAJINGA. KAMA NITAKUWA NIMEWATUSI BASI NAOMBA MNISAMEHE, ILA NINAVYOJUA MIMI, NENO UJINGA SIO TUSI BALI NI KASORO. HIVI NAOMBA NIULIZE SWALI MOJA. WAKATI UFISADI HUU WA UFUJAJI WA PEASA(EMBEZZLEMENT) UNAFANYIKA KULIKUWA HAKUNA VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU, KAMA VILE RAISI? KAMA WALIKUWEPO, KWA NINI WASIFIKISHWE KWENYE VYOMBO VYA DOLA(JUSTICE). NAOMBA MTU HUYU AKAMATWE NA KUFIKISHWA KWENYE SHERIA ILI NA SISI WANYONGE TUONE TUNATHAMINIWA MAWAZO YETU.
Monday, 23 March 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HAYA MZEE UPARA UNALO HILO, NA JK ATAKUTOA TU, NAJUA HATAKI MCHEZO NA MAFIUSADI KAMA NYIE. LOL
ReplyDeleteSURA KAMA KAMEZA SUMU
ReplyDeleteAma kweli binadamu kazi yake kutazama ubaya hata mbele ya mema mengi. Huyu aliyeacha nchi ikiwa na akiba kubwa baada ya kuipokea haina kitu, kajenga miundombinu barabara na shule na miradi kibao ya TASAF vijijini na kudhibiti mfumko wa bei nauli ya daladala na bei za vyakula, mkaa na vingi hazikupanda miaka kumi na kuja kufumka karibuni. Sawa tumhukumu tuu Mungu atamlipia!!
ReplyDeletewewe uliyeandika comentoi hapo juu hujui chochote, au huyu jamaa ni babu yako. ninahisi una matatizo ya akili wala sio bule. kwani wakati wakina sumaye wanafanya ufisadi wao nani alikuwa raisi. mimi nawashangaa sana watanzania, bado tuna utumwa wa fikra, na yatima wa siasa.
ReplyDeleteHUYU NDIYE MMILIKI WA NGURDOTO YA ARUSHA, na alishawahi kuwa na hotel south africa ila serikali ya huko iliiuza kabla nyerere hajafa na fedha kurudishwa kwa umma. je unalijua hilo au unasema tu juujuu. viongozi wetu wengi ni wanafiki tena sana tu, jam,ani watanzania tuamke. tumelala sana tu. tuamke.
KWELI WA HAPO JUU YANGU UNAONA MBALI, HEBU KAMA HAWA VIONGOZI , HASA MKAPA SI MAFISADI, ANGALIA WATOTO WAO WANANVYOMILIKI MIGODI.Watu nane wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za moto na za jadi wamevamia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira Coal Mine na kupora nyaya za umeme za kutandika chini ya ardhi zenye thamani ya mamilioni ya fedha.
ReplyDeleteMeneja wa mgodi huo, Adamu Abdu, akizungumza na Nipashe kwa simu alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana baada ya majambazi hayo yaliyokuwa na bunduki moja pamoja na mapanga na sime kuvamia mgodi na kuanza kupora nyaya hizo.
Abdu hakutaka kuzungumzia tukio hilo kwa kirefu kwa madai akuwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kyela linaweza kutoa taarifa zaidi.
Alisema majambazi hayo kabla ya kutokomea na nyaya hizo za umeme, walinzi walitoa taarifa kwa wafanyakazi na msako ulianza haraka.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa migodini na Ujenzi (Tamico) tawi la mgodi wa Kiwila, Daniel Kibona, alisema majambazi hayo yamevamia na kuiba nyaya hizo kutokana na mgodi kuwa na walinzi wachache kufuatia uongozi kutowalipa wafanyakazi mishahara kwa zaidi ya miezi nane sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen, alipoulizwa alisema taarifa za majambazi hao kuvamia mgodi huo hajazipata na kwamba atafuatilia.
Mgodi huo unamilikiwa na Nick Mkapa, Fostar Mkapa na B. Mahembe ambao wanamiliki Kampuni ya Fosnlid wakati kampuni ya Devconsult LTD wamiliki wake ni D.Yona na Danny Yonna J.R.
Makampuni mengine ambayo kwa pamoja yaliungana na kununua mgodi huo ni Choice Industries ambayo wamiliki wake ni Joe Mbuna na Goodyeer Francis na kampuni ya Universal Technologis, ambayo inamilikiwa na Willfred Malekia na Evance Mapundi.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa majambazi hayo baada ya kufanya uporaji katika mgodi huo walikwenda katika kijiji jirani na mgodi cha Lema ambako walikivamia na kuwapora wafanyabiashara wa kununua kokoa.
Wananchi wa kijiji cha Lema walifanikiwa kuwadhibiti majambazi wanne kwa kuwazingira na kuwapiga hadi kufa ambapo miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kyela.
Wafanyabiashara waliovamiwa na kuporwa na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi ni Paulo Mwambete (34), Athony Joseph (35) na Hakim Bipesa (40).
Kamanda Stephen alithibitisha majambazi hao kuvamia kijiji cha Lema na kuvunja nyumba za wafanyabiashara kwa lengo la kuwapora mali zao, zikiwemo fedha.
Alisema wakati majambazi hao wakiendelea kufanya uporaji huo, wanakijiji walipata taarifa na kukizingira kijiji kukabiliana na majambazi hayo ambayo nayo yalianza kurusha risasi.
Alisema majambazi hayo katika harakati za kujiokoa kutoka mikononi mwa wananchi waliwajeruhi kwa risasi watu sita, wakiwamo Ibrahimu Mwandubi (34), Ally Meradi (24) na Rehema Nsekeni (38) ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela.
Alisema wakati wa mapambano kati ya wananchi na majambazi yakiendelea, polisi walipata taarifa na kufika eneo la tukio na kukuta majambazi wanne wamekwishauawa kwa kushambuliwa na wanakijiji.
Baada ya kupekuliwa, alisema majambazi hayo yalikutwa na bunduki moja aina ya gobole, risasi tano, panga, nyundo na vipande vitatu vya nondo.
Mimi naona kumuongelea huyu mzee ni kupoteza muda, katiba inahitaji kubadilishwa ili kuweza kumudu ya watu kama yeye(maraisi), jambo ambalo Nyerere aliona halifai kuguswa maana anajua waliopo sasa wakiachiwa kuigusa katiba watavuruga kila tulicho nacho.
ReplyDeleteDawa ni kushika hawa wengine ambao hawana kinga wala chochote, kila nguzo ya uongozi ziwe zinajitegemea katika uendeshaji, kinachotokea sasa ni muingiliano mwingi,wanaishia kujadili tu (maprofesa) hakuna hatua za maana zinazochukuliwa.
Ushahidi upi zaidi unahitajika kushughulikia hawa akina Azizi, Lowasa, Kingunge (Pinda hongera!) Huyu Mwanyika inabidi aachie ngazi asituletee mambo ya kama vijisenti (Nae anahusika Richmond? au awajibike kikazi kama wanavyofanya nje) Mahakama zisiingiliwe, polisi inahitaji kufumwa upya kuondoa uwezo wa mtu mmoja(IGP) kuwa na nguvu. Bunge waache domo, maana ndio wanachofanyiana, kuchafuliana kama zeutamu. Serikali inayoongozwa sasa inajitahidi, lakini JK akumbuke kuna 2010 bado aliwekwa na watu na awawajibike zaidi, maana kuna mambo naona yanaendeshwa taratibu mno, mawaziri wasio na ujuzi wa kazi, kazi yao ni propaganda na kuleta masuala ya itikadi,we ukiwa na maji safi, huduma ya afya, chakula, elimu nzuri kwa familia na kazi utahangaika na chama gani kiko madarakani? Wanaweza wakadai (waendesha vyama) kuwa ndio wanachotaka kutupatia sisi wananchi lakini ukiangalia kwa undani unakuta ni kusema wanachotaka tusikie,uchaguzi ukiisha hakuna kitu.
Check and balance ni muhimu katika masuala haya, na tunapoamua kuchagua raisi hakikisha mambo aliyoyaongea JK Nyerere kuhusu raisi awe na sifa zipi. JK inabidi awe jasiri kidogo, rafiki aliye naye sasa ni huyu mzee Mkapa apende asipende, na Mwinyi pia,wao ndio wamepishana hapo,ugumu na upekwe unaohusisha hiyo kazi wanaujua, aache ujeuri aongee nao, maana kama hana watu wakaribu wanaomshauri ipasavyo, basi nahofia hakuna kitu atakachoacha katika jina lake kwa wananchi wake wenye matumaini nae (Obama US, JK Tanzania)hata kama ni mengi, alitaka mwenyewe huu mzigo.Usiku Mwema.
da. mdau mwenzangu hapo juu naona umeongea sana pinti, ila sikumalizia kwa kuwa nina kausingizi kidogo. lakini pointi yangu kubwa ni kwamba ili ufisadi usiendelee basi wakubwa kama hawa waliotusilisi nao wachukuliwe hatua za kisheria ili:
ReplyDelete1-kuwe na usawa katika jamii
2-liwe fundisho kwa viongozi wengine
3-jamii ilidhike na kuona inathaminiwa.
kama haya yote yatatokea basi nchi yetu itakua kiuchumi na kisiasa pia.
viongozi wa sisiemu wote wanafki tu. tutafanyiwa viinimacho mpaka lini? amkeni jamani. ehheeeee
ReplyDeleteMdau 26 March 2009 17:17, CCM ni kubwa mno ukianza kusema hivyo unakuwa unakosea, ni kama kusema watanzania nia wanafaki, hata kama ni ukweli, bado unakuwa unahusisha watu wengi sana.(watu watakataa unachosema baada ya hapo hata kama ni kitu cha msingi)
ReplyDeleteKazi kubwa kama za kuleta maendeleo katika nchi haziwezwi kufanywa na mtu mmoja, lazima timu ziundwe, kupigania uhuru ndio sababu ya vyama vya siasa vilianzishwa miaka ile. Ubunifu wa kutatua matatizo ya kileo ndio tatizo lililopo, hatuna mkoloni lakini bado tunanyonywa na hawa wachache (usifikiri CCM tu ndio wanaoiba).
Ugumu unakuja kuwa 'system' iliyowekwa sasa ni kwa ajili ya wachache wanaoijulia, ndio wanaokataa mabadiliko au hawako tayari kuona mabadiliko, bila ya kujua 'change is a force of nature'. Mabadiliko yalioanzishwa sasa ni mazuri lakini bado vyombo vya sheria viko nyuma vinaendeshwa kwa kujuana, sisikii mtu akiwajibishwa huku, mahakama zimechoka rushwa inanuka pindukia. serikalini watu wanaachunguzwa, wabunge nao tusiwaachie, lazima tuwape mazingira yatakayowafanya kujali zaidi wananchi wao waliwachagua kupunguza masuala ya chama. Asante. Asubuhi NJEMA
bora angesema baadhi ya viongozi wa ccm.
ReplyDeleteJAMAA NI HATARI HUYU KWA KUIBA TU. LAKINI NASIKIA JOGOO WAKE HAPANDI MTUNGI, JE NI KWELI ????????????????????
ReplyDeletekama jogoo apandi anapanda we anakuhusu nini?jogoo lake ndio litakaloiokoa yetu na ufisadi?mbu pisha uko usituletee ujinga wa zeutamu hjapa.sheria ichukue mkondo wake mh rais
ReplyDeletewe Anony wa 05:00 umetumwa nini? ila nimefurai kusikia kuwa unaijua zeutamu. hii ni kuonesha kwamba unayapenda mambo haya. but tofauti ni kwamba zeutamu blog inajihusisha saaana na maisha ya watu wa kawaida(civilian) wakati hii ya zeuchungu inajihusisha hasa na viongozi tu, tena wale mafisadi. u better know.
ReplyDeleteJAMANI WATANZANIA MIMI NAONA TUTAONGEA SANA KUHUSU HAWA VIONGOZI MAFISADI, LKN SWALI LANGU NI MOJA TU.
ReplyDeleteJE TANGU SERIKALI YETU IMECHUKUA MADARAKA NA KUWA NA RAISI WAKE WA KWAMBA JK NYERERE KUNA KIONGOZI YEYOTE AMBAYE AMESHAWAHI KUFUNGWA KUTOKANA NA KOSA LOLOTE LILE?
KAMA YUPO BASI NAOMBA JINA LAKE.KAMA HAYUPO BASI NDIYO UJUE JINSI GANI TANZANIA KUSIVYOKUWA NA SHERIA YA KWELI.