Wednesday, 8 April 2009

MH. JK UNAYAJUA MAMBO WANAYOFANYIWA WANAFUNZI WA KITANZANIA WA HUKO URUSI?

nduGu yetu Bw. zeuchungu sisi ni baadhi ya wanafunzi ambao tuko huku URUSI kwa ajiri ya masomo lakini jinsi tunavyofanyiwa na ubalozi huu wetu wa huku chini Ya bw. JAKA MWAMBI kwa kweli ni kinyume na haki za binadamu na ni manyanyaso.
Hali tuliyonayo huku ni mbaya kuliko maelezo yaani kazi hakuna, hata ya kuokota mawe na hawa viongozi wetu ubalozini hawajishughulishi na sisi katika kuhakikisha tunapata mahitaji yetu tukiwa kam watanzania na wanafunzi.
SASA JE SISI TUTAJIVUNIA NINI KUITWA WATANZANIA?
JE HIVI NI KUTUSAIDIA AU KUTUPOTEZA KIMAISHA?
TUTAWEZAJE KUJIKIMU NA HALI NGUMU YA MAISHA IWAPO HATUNA PESA?
JE HALI HII ITAISHA LINI?
JAMANI NAOMBA MFIKISHIANE UJUMBE ILI HABARI HII ITOLEWE KWENYE MAGAZETI NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI ILI TUWEZE KUSAIDIWA . NDUGU ZETU WADAU TUNAWAOMBA SANA KWA HILI.
ASANTENI.

25 comments:

  1. asante saaaaaaaaaaaaaana bwana zeuchungu najua habari zitamfikia tu mh. JK

    ReplyDelete
  2. Je kwanini msirudi BONGO?

    ReplyDelete
  3. Annony 21:58 nakuunga mkono 100%,sielewi hawa jamaa wanalalamika kitu gani,si warudi bongo kama wao ni wazalendo wa kweli.Ndio hawa hawa wakishamaliza chuo wanang'angania kubaki huko huko wanasahau kama pesa zilizowasomesha ni za wakulima wa huku bongo.Rudini bongo tuijenge nchi yetu! Mtasoma huku huku home vyuo vipo vingi vya kumwaga!! Siku ya kurudi mtuambie tuje kuwapokea airport mashujaa wetu mliopigania haki za wanyonge...kilio chenu kimesikika na waliobaki watatendewa mema kama mlivyokuwa mkihitaji!! Hayo ndioo maisha ndugu zangu! Remember life is not a reharsal its a perfomance..changanyeni karata zenu vizuri na mlambe dume before its too late.Muda unaenda ndugu zangu tangu nianze kusikia sakata lenu ni karibu waka sasa kama mngeamua kurudi huku si mngekuwa mko mbali sana.

    ReplyDelete
  4. mdau mwenzangu wa hapa juu yangu nimegundua ya kwamba wewe unaweza ukawa mmoja kati ya hawa mafisadi. anyway mimi ninasomea saikilojia huku UK lakini nimegundua ya kwamba umetoa komenti nyingi sana kwenye hii habari.
    Kitu ambacho napenda kukuambia ni kwamba unawavunja sana moyo hawa vijana na kwa kweli sidhani kama kuna msaada wowote unaoutoa ili kuwasaidia.
    Suala zima la kurudi bongo sio suluhisho la matatizo kwani hata bongo kusoma ni shida vilevile ila nachoona mimi ni kwamba kwa kuwa serikali imejitolea kuwasomesha vijana hawa basi itabidi iwajibike kwani nikisoma habari hii ninaona kama vile wqametelekezwa.
    NAJUA SERIKALI NDIYO WAAMUZI WA SUALA HILI LAKINI ISITUMIE NGUVU KTK KULITATUA TATIZO BALI ITUMIE BUSARA INAYOENDANA NA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU. KAMA VIJANA HAWA WATALALAMIKA KWENYE SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI BASI SERIKALI YETU NA VIONGOZI WAHUSIKA WATAKUWA MATATANI.
    NISESOMA KATIKA HABARI NYINGINE HAPA CHINI ETI WANAZUNGUMZIA SUALA LA ULEVI.
    HEBU NIWAAMBIE KIDOGO ULEVI NI KITU AMBACHO KINAJITOKEZA KWA NAMNA MBALIMBALI UNAWEZA KUWA MLEVI KUTOKANA NA KUTAKA KUPUNGUZA MAWAZO AU KUNA UPATIKANAJI WA POMBE NYINGI MAENEO UNAYOISHI.
    LAKINI mbona watu huwa wanalewa na wanajua wanachokifanya? kuna madokta hospitalini wanalewa kabla ya kufanya upasuaji.
    mimi naona suala la ulevi ni kitu cha kawaida kwa binadamu japo ukizidi huleta madhara.
    NINGEPENDA KUMALIZIA KWA KUSEMA KWAMBA VIJANA HAWA WASAIDIWE ILI WAENDELEE NA MASOMO NA KAMA KWELI WAPO WALIORUDISHWA BONGO BILA SABABU YA KURIGHISHA BASI NA WAO WARUDISHWE TENA HUKO URUSI ILI WAENDELEE NA MASOMO.

    YA MWISHO KABISA NINGEPENDA KUSEMA "NO PAIN NO GAIN"

    ReplyDelete
  5. Poleni sana ndugu zangu kwa yaliyowapata!! Naamini kiliochenu kitasikika!!! Bongo Ufisadi mtupuuuuu!!!!

    ReplyDelete
  6. Jamni kiswahili ni kigumu!!! Nimeomba mniambie haki mlizokuwa mnazipigania hamtaki.Kaazi kweli kweli.Anyway kwa msaada zaidi nimeleka mjadala huu kwa Michuzi huenda mkapata ushauri mzuri zaidi kwenye blog hiyo.Keep in touch!!! Mimi wala sio fisadi kama unavyodhani ila ni mtu wa Principles!! Na ni mtu ninayetumia akili yangu kupata mkate wangu wa kila siku....Siwaonei wivu Mafisadi na walas= siwafagilii vilevile.

    ReplyDelete
  7. WAT I KNOW IZ DAT PEOPLE THEY don’t shade blood without reason, so THERE MUST BE SOMETHING BEHIND

    ReplyDelete
  8. whats goes around come around nahisi hili suala litawatokea hawa wanyanyasaji kama ni kweli wamelifanya hilo.

    ReplyDelete
  9. A dog should never bites its owner even it's mad.

    ReplyDelete
  10. JK hana muda wa kuangaika na hawa watoto ana mengi ya kufanya

    ReplyDelete
  11. wewe hapa acha kuwa limbukeni namna hiyo JK yupo kwa ajiri ya watu wote na sio wachache tu.

    ReplyDelete
  12. JAMANI MBONA KILA MTU ANASEMA YA KWAMBA JK NDIYE ANAYETAKIWA KUSHUGHULIKIA SUALA HILI. KWA KWELI JK NI MTU AMBAYE LABDA NISEME YUKO BIZE SANA NA MAMBO MAKUBWA YA KISERIKALI NA SUALA KAMA HILI KUMFIKIA NI KAZI SANA.
    LAKINI HAKUNA BALOZI HUKO URUSI ILI ASAIDIA HILI AU HATA VIONGOZI WA NGAZI NYINGINE PIA KULIKO JK.
    PIA NADHANI HATA SISI WANANCHI TUKITOA KAULI KALI NADHANI HAWA MAFISADI WATAACHA TABIA YAO CHA MSINGI NI KUUNGANA TU NDIYO SURUHISHO.

    MCHANA MWEMA
    K USA

    ReplyDelete
  13. JK JK JK JK UKO WAPI RAISI WETU? TUOKOE WANAO

    ReplyDelete
  14. JAMANI NYIE SI MRUDI HUKU NYUMBANI MTATAFUTA SHULE NYINGINE, AU MNATAKA MUOE NA KUOLEWA UKO UKO?

    ReplyDelete
  15. semeni semeni vijana msiogope hawa watu wanatuchezea sana kiasi ya kwamba tumeshindwa kuvumilia watu tunajitoa muanga tu. kumamamae

    ReplyDelete
  16. CIKILIZENI VIJANA WANGU UJUE SERIKALI YETU WENGI WALIOKUWEPO MADARAKANI NI WATU WAZAMANI MNO HAWAELEWI MAMBO NA WANAPELEKA MAMBO KIZAMAN ZAMANI,MIMI NAIMANI KABISA SERIKALI KABLA HAIJAPELEKA HAWA WANAFUNZI HAIKUFANYA UTAFITI WAKINA WAMAHALI WANAPO WAPELEKA ILA WALIKURUPUKA NA KUTAKA SIFA KWAMBA WANASOMESHA WANAFUNZI WENGI NJE YA NCHI MATOKEO YAKE NDIO HAYA.SASA BASI SERIKALI INGESTOPISHA KUREPELEKA WANAFUNZI HUKO URUSI THEN WAWA UDUMIE WALIOBAKI MPAKA WAMALIZE, KWA AKILINDOGO HAWA WALIOPO HUKO WANALALAMIKA THEN SERIKALI MWAKANI WATAPELEKA TENA WANAFUNZI SASA AKILI HIYOOO?NDO MATOKEO YAKE WANASHINDWA KUWAUDUMIA KUMSOMESHA MWANAFUNZI NJE NI GHARAMA KUBWA SANA NA UNAPO PANGA KUMSOMEHSA KAMA NI SERIKALI HUWA KUNA MIKATABA SASA INABIDI UJUE MPAKA MWANAFUNZI MMOJA ANAMALIZA ATA COST SHL NGAPI HAPO HUTO PATA TABU NADHANI SERIKALI YETU HALITAMBU HILO ILA INATAKA SIFA2,NA NYINYI WANAFUNZI MNAOTAKA KWERNDA KUSOMA NJE KAMA BABAYAKO HANA UWEZO KABISAAAA BOLA UBAKI NYUMBANI USOME NYUMBANI MSAADA WA WAZAZI HUKO KAMA MDOGO UTAPATA TABU MATOKEO YAKE NDO HAYA

    ReplyDelete
  17. Ushauri wa bure! andikeni majina yenu na habari hii yote..pamoja na statement from your univerisity head..official statement on headed paper..alafu upload hapa watu tulipue magazetini bongo...kama mnataka haki itendeke msilalamikie JK..seek sympathy from the tanzanian public through the media sio zeuchungu or blogs..mkilipua hii habari kwenye magazeti..mtaona ubalozi wa urusi utavyohahaha..stand together and get this done..lakini muwe na facts! hata warecodini hao wafanyakazi wa balozi hata balozi mwenyewe akiwanyima haki..it will make your case stronger than kuja hapa na kulia.

    ReplyDelete
  18. Afadhali anony hapo juu,maana mie nimejaribu kuwachimba hawa jamaa angalau waeleze kwa muhtasari masahibu yaliyowakuta hawataki wameishi kunihisi huwenda na mimi ni FISADI any way nshawasamehe,najua stress sometimes zinaweza kufanya ufikirie ndivyo sivyo!! Toeni yaliyo ya kweli na yenye facts ili tuyaanike magazetini huku bongo,otherwise yataishia humu humu.

    ReplyDelete
  19. guys don trust no one hakuna haja ya kuyaandika majina ya victims wa suala hili na cha kufanya ni kutuma malalaniko yenu kwenye uongozi wa wizara ya elimu na mikopo ya serikali. i will come bac soon with the full address so u can post ur claims through. don worry guys but msiyatoe majina yenu kwani inawezekana wanoandika hizi coment za kuhitaji majina ndiyo hao hao. b careful.

    mdau wenu.

    ReplyDelete
  20. Kweli mdau hapo juu anon. 18 April 2009 07:13 , msiandike majina yenu hapa, maana viongozi wengine hawapendi kusemwa kama wanachemsha, lakini bado nasema jipangeni vizuri mueleze hoja zenu vizuri, msitahamaki wala kuvunjika moyo, msiache kupigania haki zenu.

    Hili suala inawezekana likawa linahitaji uchunguzi zaidi, maana sioni kuona maana ya watu kumtupia maneno makali japokuwa sio matusi huyu mzee anayemwakilisha raisi huko Urusi bila ya kuwa na sababu za msingi. Hali ya sasa sio nzuri kila mtu analinda kijikazi chake alichonacho, JK ni mwanasiasa pia, leo kesho anaweza akaamua kumbadilisha akiona anaharibu huko, kwa hiyo kama kuna jambo kweli ninyi msiache kulisema, atashughulikiwa tu. Jamani nimechoka kuongelea hili suala, nawatakia jioni njema.

    ReplyDelete
  21. wajinga ndio waliwao kama mtalalamika tu bila kueleza kinagaubaga basi mtaishia kwenye mateso na mwisho wake ni kuanguka.,

    ReplyDelete
  22. jamani kikwete ni fisadi kama hawa na hawezi kusema wala kuanya lolote kuhusu suala hili yeye anahusika na madili makubwa makubwa tu,

    ReplyDelete
  23. Kwani mlipoponda pipa kwenda huko urusi hamkujua jinsi mtakavyoishi? Wacheni kupiga kelele za hovyo kuna watu bongo hata nafasi ya kusoma hawapati nyie mnaleta za kuleta wasenge au? Watu kibao home hawana maji safi na salama nyie mko huko majuu mmeshiba na kucheua manguruwe na makuku sasa mnataka pesa za kununua TV? Acheni usenge wenu someni mmalize mrudi kulima hakuna kukaa mjini mrudi kwenu shambani kenge nyie

    ReplyDelete
  24. safi sana anony 30 April 2009 13:42,watu wenyewe hata hawasemi wananyanyaswa vipi? Labda wanayimwa hela ya kwenda kwenye Casino....!!!!!

    ReplyDelete
  25. kwanini URUSI mbona tuliochina serikali inatushughulikia vizuri tu! tena mkapa alikuwa natupenda sana akija beijing kikwete alipoingia akabadili mambo kibao tulichofanya alipokuja kutembea china ubalozi ukatuita wanafunzi wa TZ wote.. lakini tukagoma na tukatuma barua! wakarekebisha mambo!
    hongera ubalozi wa tanzania china

    ReplyDelete

SEMA USIOGOPE, JAMII INAKULINDA.